Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr and Sheikh Nasir Khamis Tafsiri: Az-Zumar Ayah 72

39:72
قيل ادخلوا ابواب جهنم خالدين فيها فبيس مثوى المتكبرين ٧٢
قِيلَ ٱدْخُلُوٓا۟ أَبْوَٰبَ جَهَنَّمَ خَـٰلِدِينَ فِيهَا ۖ فَبِئْسَ مَثْوَى ٱلْمُتَكَبِّرِينَ ٧٢
قِيلَﲘ
ٱدۡخُلُوٓاْﲙ
أَبۡوَٰبَﲚ
جَهَنَّمَﲛ
خَٰلِدِينَﲜ
فِيهَاۖﲝﲞ
فَبِئۡسَﲟ
مَثۡوَىﲠ
ٱلۡمُتَكَبِّرِينَﲡ
٧٢ﲢ
Itasemwa: Ingieni milango ya Jahannamu mdumu humo. Basi nayo ni ubaya ulioje wa makaazi ya wanao takabari! 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na wataambiwa wale wenye kukataa kuwa Mwenyezi Mungu Ndiye Mola wa haki, kwa kuwatweza na kuwadhalilisha, «Ingieni kwenye milango ya Jahanamu, hali ya kukaa humo milele.» Ni mbaya mno mwisho wa wale wanaolifanyia kiburi jambo la kumuamini Mwenyezi Mungu na kufuata kivitendo sheria Yake.